Wakazi wa Mwanza wafundwa amani uchaguzi mkuu

MWANZA: ZIKIWA zimebakia siku tisa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, wakazi wa Mkoa wa Mwanza wameshauriwa kudumisha amani pamoja na kutambua umuhimu wa kupiga kura na kutambua kupiga kura ni wajibu wao kikatiba.

Hayo yamesemwa leo na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke wakati wa kongamano la amani la viongozi wa dini mbalimbali.

Amesema amani itasaidia kuvuka salama wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Amesema ni vyema kuchagua viongozi sahihi watakaosaidia katika kuendeleza na kudumisha amani.

Naye Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza, Charles Sekelwa amesema kupiga kura ni haki ya kila mtu hivyo ni vizuri wakazi wa Mkoa wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla kuangalia sera zote za wagombea na kwenda kupiga kura.

“Oktoba 29, tutoke na kwenda kupiga kura pia tuacha tabia ya kushawishiana kuwa Watanzania wasiende kupiga kura jambo ambalo sio sahihi. Pia watu wasiwe na lengo la kuharibu kura,”amesema.

Amesema Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza imetoa tamko na kuahidi kuwa itaendelea kuhamasisha upigaji wa kura wa Uhuru na haki kisha kurejea majumbani kwao.

“Tunawahimiza wananchi wote kutumia haki yao ya msingi kumchagua rais, wabunge na madiwani katika ngazi zote kwa upendo, busara na uwajibikaji” mwisho.

Amesema baada ya kumaliza zoezi la kupiga kura, kamati ya amani ya mkoa inawasii warejee majumbani kwao kwa utulivu bila vurugu na bila maneno ya chuki.

Naye Waziri Mstaafu, Lazaro Nyalandu amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuungana kwa pamoja katika kudumisha amani. Amewaomba viongozi wa dini waungane kwa pamoja katika kuiombea amani nchi ya Tanzania pamoja na kumuombea Rais wa Tanzania.

Amewaomba Watanzania wote kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura siku ya Oktoba 29.

Amesema Watanzania wakumbuke amani ni nguzo ya maendeleo, umoja ni nguvu na upendo ni suluhisho la kila changamoto hivyo kuviombea vyombo vyote vinavyosimamia uchaguzi, Mungu avijaalie hekima na uadilifu pamoja na uaminifu katika majukumu yao.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button