Wanaochezea mapato ya serikali kuchukuliwa hatua

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marko Ng’umbi kuchukua hatua kwa wale wote wanaochezea mapato ya serikali ikiwemo leseni za biashara na mfumo wa mapato ya ndani wa “POS ”

Mongella ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani wilayani Longido wakati wa kujadili Utekelezaji wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na Maagizo ya Kamati ya Bunge la Laac kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Amesema kunawatumishi wanacheza na mifumo ya serikali kwa kuiba fedha mbichi katika mfumo wa mapato ya ndani ya “POS” ambayo hayajawasilishwa benki yenye thamani ya Sh milioni 13.

Advertisement

Lakini pia leseni za biashara napo kunamchezo wafanyabiashara wanapewa leseni kumbe leseni hizo hazijatolewa na Brela wala hata walipofuatilia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa Ofisa Biashara Mkoa hakukuwa na vitabu vilivyotoka vya leseni na hata kwa mpigachapa mkuu wa serikali haikuonyesha nyarakaza vitabu hivyo kuchapwa.

“Longido kunamapato lakini kunawatu wanacheza na hizi hela mbichi na hapa ndipo kunaupigaji mkubwa sana sasa sitaki kusikia fedha mbichi zikiliwa DC, chukua hatua katika hili kunawatu wanacheza na hela za leseni ya biashara na ukiona mtu anachezea mfumo kamata weka ndani”

Amesema mapato ni injini ya halmashauri lakini kunawatu wanacheza na hizi leseni na wengine wanakula hela mbichi hivyo kila anayekula hela mbichi achukuliwe hatua hapa Longido kunageti la ushuru lakini kwanini magari yapite mengi mapato yawe kidogo hapa kuanmchezo unafanyika Dc chukua hatua

Awali Mkuu wa Wilaya ya Longido,Marko Ng’umbi amekiri wilaya hiyo kuwa na wizi wa leseni halisi za biashara na wamelifuatilia jambo hilona walibaini kunavitabu vya leseni za biashara zilitolewa leseni pasipo kufuata taratibu na tayari Ofisa biashara wa awali anayeitwa Paulo Parmeti amesimamishwa kazi kwaajili ya kupisha uchunguzi huo.

“Nitachukua hatua katika hili maana kunawatu ukianza kuchukua hatua madiwani wanapiga kelele nyingi sasa katika hili nitachukua hatua maana hapa Longido tunaminada na maeneo mengine ya ushuru lakini tumebaini ukiweka mtumishi wa serikali kutoka taasisi Fulani mapato yapo juu,ukisema uwaachie wanaosimamia mapato yanashuka hii sitaikubali ”

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido, Stephen Ulaya alisema wilaya hiyo inajumla ya hoja 48 za miaka ya nyuma 2015/2016 hadi 2020/21/22 ambapo hoja 20 zilitekelezwa huku hoja 28 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *