Wanasheria mnawajibu kuitetea Serikali- Mchengerwa

DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema wanasheria wote walioko katika sekta ya sheria wanapaswa kujua wanawajibu wa kuitetea na kulinda Serikali dhidi ya maadui wanaoweza kuihujumu serikali.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.
Pia amewataka kuwa wazalendo, waadilifu, kufanya kazi kwa weledi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani Serikali ikianguka wote tutakuwa tumeanguka.
 
Aidha, ameiomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa karibu na wanasheria wa mamlaka za serikali za mitaa ili kusaidia uboreshaji wa sheria ndogo na kanuni zinatotumika kwenye halmashauri.
“Kwa sasa kumekuwa na malalamiko ya kuwapo sheria ndogo na kanuni ambazo hazizingatii katiba na sheria mama hiyo kuwatesa wananchi hususani wa vijijini hivyo mkaziboresha kuondoa malalamiko,”amesema Mchengerwa.
Awali, Mwenyekiti wa Baraza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk Eliezer Feleshi alisema Ofisi yake ina upungufu wa watumishi 285 huku asilimia 85 ya watumishi waliopo wamepatiwa vifaa vya TEHAMA hivyo kupunguza mrundikano wa shughuli mezani na kurahisisha uendeshaji wa mashauri kwa njia ya mtandao.
 
Alisema pia wanasheria 3,359 wamesajiliwa kwenye mfumo wa Chama Cha Mawakili wa Serikali na kati ya hao wanasheria 307 ambao ni asilimia 9 wako kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button