Wanasiasa wachonganishi hawafai -CPA Makalla

ZANZIBAR: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka watanzania kuachana na viongozi fitna na wachonganishi kwani wanaleta chuki na uhasama hata pale mazuri yanapofanyika

Maneno hayo yametolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla wakati akizungumza na Wananchi na wanachama katika Viwanja vya Umoja ni nguvu kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 6 Visiwani Zanzibar.

“Sisi CCM tutetembee kifua mbele kazi ya kuwahudumia Wananchi wale wenzetu ni watu wa vituko ,uongo, fitina na majungu ndo kazi yao sisi tunajukumu na dhamana ya kuwaletea Wananchi maendeleo,” amesema Makalla.

Aliongeza:”Nayasema ivi kwasababu wanakuja hapa wanasema mnajenga maghorofa wakati watu wanakufa na njaa na miradi yote sio maendeleo sasa ndo ujue kuna shida na anaetamka hayo ni mtu mzima ndo mana nasema kazi ni kusema uongo na vituko lakini hawo hawo Viongozi ndugu zao wanasoma katika hayo maghorofa na wanapata huduma mbalimbali lakini hawazioni niseme muda wa kudanganyana umeisha pamoja majukumu walilojipa tuwaogope Viongozi fitina.”

Mwenezi Makalla ameendelea kusema kuwa Samia Suluhu Hassan na Dk Hussein Mwinyi hawana ubaguzi wowote kwenye suala la kuwaletea maendeleo lakini wenzetu kila kukicha wanaweka fitina na hili kazi kwenu Wazinzabar kwa ujumla wakataeni Viongozi hao na wanasiasa hao kwa kuwanyima kura wakati Uchaguzi utakapofika na tuchague chama cha mapinduzi ambacho ndo kina wajibu wa kuyaleta.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button