‘Wanasiasa wajiepushe kauli kuvuruga amani’

DAR ES SALAAM; mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, amewataka wanasiasa nchini kuacha mara moja tabia ya kuzihusisha klabu za Simba na Yanga na masuala ya kisiasa, akisisitiza kuwa jambo hilo linaweza kuchochea migogoro isiyo ya lazima katika tasnia ya michezo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Steve amesema kuna ongezeko la wanasiasa wanaotumia majina ya klabu hizo maarufu kwa manufaa ya kisiasa, hali ambayo italeta mgawanyiko usiokuwa wa lazima kwa mashabiki wa soka na taifa kwa ujumla.

“Hizi ni timu kongwe, zimekuwepo kabla hata mimi sijazaliwa. Halafu unakuta mwanasiasa anasema, ‘kama ningekuwa Rais, ningezifuta Simba na Yanga.’ Hii ni hatari kwa mustakabali wa michezo nchini,” amesema.

Pia amewaonya baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa wakitumia nyumba za ibada kutoa matamko yenye mlengo wa kisiasa, akisema ni kinyume na maadili ya kiroho na kunahatarisha mshikamano wa kitaifa.

“Kuna mmonyoko mkubwa wa maadili katika jamii, lakini cha kushangaza, viongozi wa dini hawakemei hayo, badala yake wanatumia madhabahu kuzungumzia siasa. Hii siyo sawa na ni hatari kwa amani ya taifa letu,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button