Wanatuita maskini huku ‘wanakuja kula kwetu’!
VURUGU zilizotokea nchini Oktoba 29, 2025 iliyokuwa siku ya uchaguzi mkuu na siku kadhaa baadaye, ni kosa lililofanywa na baadhi ya Watanzania huku wengi wao wakiwa hawajui kuwa, wanatumiwa kuangamiza nchi yao kwa kudanganywa na watu wanaotuita maskini, huku ‘wanakuja kula kwetu.’
Ndio maana Watanzania wanaoipenda Tanzania yao na watu wake, hawatachoka ‘kusema na kusema’ na kisha kurudia kusema kuwa, tulikosea na tujue tulikosea wapi ili tusirudie kosa maana kosa ni hasa kurudia kosa na si kufanya kosa na kupotea njia, ndio kujua njia.
Hili la Oktoba 29, 2025; siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani halitaachwa kusemwa ili watu wajue kuwa, waliowadanganya, hawakuwadanganya kwa kuwa wanawapenda, bali kwa kuwa wanataka kuwatumia kama chanzo cha mapato yao wanapotumikia hao wanaotuita maskini huku wanataka kuja kwetu.
Ndio maana mara kwa mara kwa uchungu kabisa na kwa kuona watu wa Mungu wanaangamiza nchi na ‘kuchoma nyumba’ yao kwa kukosa maarifa, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba anafichua ukweli. Anasema, yaliyotokea Oktoba 29, hayakuwa maandamano, bali hujuma za kiuchumi dhidi ya Tanzania.
Hujuma hizo kimsingi zinalenga kuona wakati Watanzania ‘wanamwagiana damu’, wao waje ‘kula na kunywa’ uchumi wa Tanzania hadi ‘washibe na kutapikia soksi.’ Maskini! Watanzania hatukujua kuwa tunazolewa na kukataa pazuri bila kujua kuwa tunapelekwa pabaya panapotuita.
Ee Mungu! Tunaomba utasamehe kwani tumekosa mno kushiriki kwa mikono yetu kujihujumu kiuchumi nchi yetu maana uchumi na maendeleo ya Tanzania, ni mali yetu Watanzania. Katika hotuba zake maeneo mbalimbali ya nchi, Mwigulu anafumbua macho ya Watanzania na kuwapa fikira tunduizi anaposema: “Tanzania inapigwa vita ya kiuchumi kupitia Watanzania wachache wenye nia ovu dhidi ya taifa lao.”
SOMA: Tume kuchunguza mambo 6 vurugu za Okt.29
Hao, ni wale wanaotaka kuwa vibaraka wa mabeberu wanaoziita nchi za Afrika kuwa ni maskini, lakini wanataka kuja kula kwetu Afrika. Anasema: “Watu hao (mabeberu) wanatazama rasilimali… Ndivyo walivyofanya kwa wenzetu maana wao wanawapa mabomu wao wanachukua rasilimali zilipoisha, wanaacha kuwachonganisha.”
“Niwahakikishie wanaomezea mate Tanzania kwamba, tutalinda Tanzania kwa gharama zote na Tanzania haitaendeshwa kwa rimoti,” alisema.
Kwa tafsiri nyepesi ya asemacho Waziri Mkuu Mwigulu ni kuwa, kama wanavyofanya katika nchi nyingine za Afrika hasa zenye utajiri wa rasilimali mbalimbali yakiwamo madini ya aina mbalimbali kama dhahabu, almasi, tanzanaiti (ipo Tanzania pekee), gesi asilia, makaa ya mawe na chuma, ndizo zinazochonganishwa na kuingizwa kwenye migogoro.
Wanachonganisha Watanzania ili kama wanavyofanya katika nchi nyingine walizofanikiwa kuhujumu
na kuchonganisha, ili wakati tunamwagiana damu, wao wachote dhahabu, almasi na vito vingine vya thamani
waende navyo kwao huku wakijidai kulinda amani na kutoa misaada.
Kwamba, giza la Watanzania kumwagiana damu linapoingia, wao wafurahie na kutuuzia silaha kwa bei na masharti wanayotaka.
Kisha wapandishe bei ya bidhaa mbalimbali tunazohitaji maana hatupati muda wa kuzalisha, bali wa kutumia kinachopatikana kwa shida au kwa kupewa na wenye huruma kwani mnapoingia katika vurugu, hakuna muda wa kufanya shughuli za uzalishaji mali kama kilimo wala biashara.
Turejee na kukumbuka siku kadhaa za zuio la kutoka nyumbani baada ya vurugu za Oktoba 29; namna watu walivyoteseka kwa kula wasichozalisha na kisha wengine wakaishiwa na kubaki na fedha mkononi maana fedha haziliwi. Zilizokuwa benki; hakuna namna ya kuzifikia; ni shida tupu maana ‘mchuma janga hula na wa kwao.’
Dk Mwigulu anaweka bayana kuwa hujuma hizo za kiuchumi dhidi ya Tanzania zinakuja baada ya Tanzania kutaka kuanza mradi wa gesi asili mkoani Lindi utakaofanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi wazalishaji wakubwa duniani.
Aidha, zinakuja huku mradi wa makaa ya mawe na chuma ukiwa unaiweka Tanzania miongoni mwa nchi tano wazalishaji wakubwa wa rasilimali hizo (chuma na makaa ya mawe).
Kimsingi, Oktoba 29, 2025, Watanzania tulikosea ‘tukaingia mkenge wa wajanja wachumia tumbo’ walio tayari kuona taifa linateseka na watu wake wakiwamo, ndugu, jamaa na marafiki, mradi tu wapewe zawadi na ‘watoka mbali’ wanaotuita maskini, huku wanakuja kula kwetu.
Tulikosea kwa sababu yaliyotokea Oktoba 29, si maandamano, si siasa, si demokrasia, wala suala la haki za binadamu, bali kweli ni hujuma za waziwazi dhidi ya Tanzania zinazofanywa na wanaotuita maskini, huku wanatamani utajiri wetu.
Kimsingi, hawafurahii kuona taifa hili likiwa limejaliwa rasilimali nyingi na watu wake wengi (nguvukazi katika uzalishaji mali); hawafurahii kuona tunakamilisha mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere
(JNHPP), hawafurahii kuona tunazidi kununua na kujenga miundombinu ya huduma mbalimbali zikiwamo za
usafiri kama Reli ya Kisasa (SGR) kwa fedha zetu wenyewe; hawafurahii kabisa.
Hawafurahii kuona tunatumia kwa tija vivutio vya utalii na uwekezaji ambavyo kwao havipo na wanavitamani na kubwa zaidi, hawafurahii kuona Tanzania inazidi kutajirika kwa madini mbalimbali yanayozidi kupatikana nchini yakiwa na thamani kubwa na mengine hayapatikani kwingine kote duniani.
Ndiyo maana Watanzania wameshituka na katika kada na nafasi mbalimbali, wamegundua kuwa walizolewa na kudanganywa ili wawe watumwa wanaojipeleka utumwani. Kwamba, hujuma hizo ni vita ya uchumi inayotumia kanuni ya kuvuruga watu na kuwagawa, ili uwatawale vizuri ama iwe kisiasa, kijamii au hata kiuchumi.
Kuthibitisha kuwa, ‘tulichotwa na kuzolewa’ na kutupwa kwenye janga huku tukidhani tunapendwa na tunajua kudai haki kumbe tunaharibu njia za kudai haki, tujiulize kila mmoja kwa nafasi yake kwamba, madhara ya miundombinu tuliyoharibu kwa akili na mikono yetu yamemkumba nani kama si kwamba, tulipiga ngumi kwenye ukuta tukaumiza mikono yetu!
Novemba 25, 2025 wakati anazungumza na wahariri na waandishi wa habari Dar es Salaam, Dk Mwigulu anasema miundombinu iliyoharibiwa ni ile inayotumiwa na kila Mtanzania kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii nchini.
Anasema: “Miundombinu hii si mali ya serikali, zahanati si mali ya serikali, barabara pia hivyo hivyo ni mali ya Watanzania maana imejengwa kwa fedha za Watanzania ndiyo maana hata ukinunua shati la mtoto wako mchanga, ipo sehemu unachangia miundombinu hii…”
Ndio maana wadau wa amani na maendeleo nchini wanasema, Mwaka 2026 uwe mwaka wa marekebisho na kujenga amani, maelewano na kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi maana Tanzania ni yetu, hakuna atakayetusaidia kuijenga, bali wapo wanatamani kutusaidia kuibomoa ili watufanye watumwa wao wa kiuchumi na pengine hata kisiasa.




l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com