Wanawake Tehama watakiwa kutatua changamoto za jamii

MHADHIRI kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dk, Neema Mduma ametoa wito kwa wanawake walio katika sekta ya TEHAMA kutumia ujuzi wao kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Dk,Neema ametoa rai hiyo katika mahojiano maalum na televisheni Mtandao ya TCRA kupitia mada ya ujasiriamali kupitia Tehama.

” Natoa wito kwa wanawake wenzangu waliopo katika sekta ya TEHAMA kutumia teknolojia ili kuleta maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii”.

Ameeleza kuwaTaasisi ya Nelson Mandela ipo mstari wa mbele katika kuwainua sekta ya TEHAMA kupitia CENIT@EA imeweza kufadhili wanafunzi kutoka nchi za Afrika Mashariki kupata elimu na ujuzi katika sekta hiyo.

Pia ametoa mfano wa wanawake watatu ambao wamechangia katika ujasiriamali kupitia TEHAMA ambao ni pamoja na Dk Dina Machuve – mmoja wa waanzilishi wa Asasi isiyo ya kiserikali ambayo imelenga kutumia teknolojia ya mashine ya kujifunzia ( Machine Learning) katika kutatua matatizo mbalimbali ya jamii.

Ametaja kuwa ni kutengeneza mifumo ya kugundua magonjwa yanayoshambulia kuku na kutafuta suluhisho na Rose Funja Mkurugenzi na Muanzilishi wa Agriinfo ambayo imelenga kutumia teknolojia ya drones au ndege zisizo na rubani katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba wakulima .

Vilevile, Carol Ndosi Mwanzilishi wa the Launchpad Tanzania ambae amejikita katika kusuka agenda ya mitandao salama na wanawake katika teknolojia.

Habari Zifananazo

Back to top button