“Wanawake tunapopata fursa tutende haki”

MKURUGENZI wa Ununuzi Wizara ya Nishati, Marieta Kiago amewashauri wanawake hususan vijana kuwa wanapopata nafasi za kufanyakazi kwenye maeneo au taasisi mbalimbali kuhakikisha wanasimama imara na kutenda haki kwa wananchi.

Kiaho ameyasema hayo wakati akielezea nafasi ya msichana katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mkoani Arusha.

“Ninachotaka kusema katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani wale tunaopata nafasi basi  tuzitendee haki hasa tunapotoa huduma kwa wananchi,” amesema Kiago.

Akizungumzia  kuhusu usawa, Kiago amesema  unatakiwa kuwepo katika jinsia zote kwa wanawake na wanaume ambapo ameipongeza serikali kwa kuweka usawa katika utekelezaji wa majukumu kwenye jamii.

Ameongeza kuwa kwa sasa wanawake wengi wameshika nafasi mbalimbali za uongozi akitolea mfano Rais Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button