Wanawake, vijana kunufaika nishati safi

ZAIDI ya wanawake na vijana 1,500 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya nishati safi kupitia mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika la Maendeleo ya Kijamii (REDESO) kwa kushirikiana na vyuo sita vya VETA nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa warsha ya kujadili utekelezaji wa mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa REDESO, Abeid Kasaizi amesema  mradi huo unalenga kuandaa mitaala ya kozi fupi na ndefu kadhalika na kuvijengea  uwezo wa vituo vya mafunzo, kupanua wigo wa wanufaika na kuhakikisha uendelevu wake kupitia mifumo ya VETA.

Amesema mradi huo ulianza kwa majaribio uliowahusisha wanawake na vijana 500 na sasa umepanuliwa kufikia wanufaika 1,600, hatua inayolenga kuwajengea uwezo katika sekta ya nishati jadidifu. SOMA: Viongozi wahimiza uwekezaji nishati jadidifu Afrika

Kasaizi ameeleza kuwa mafunzo hayo yatahusisha teknolojia mbalimbali za nishati safi ikiwemo majiko banifu, mifumo ya sola na usafiri wa umeme, pamoja na mafunzo ya ujasiriamali ili kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kuanzisha biashara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Wilhard Soko amesema mafunzo hayo yanalenga kuandaa mitaala inayozingatia mahitaji ya soko la ajira na kuwawezesha vijana na wanawake kupata ajira katika sekta ya nishati jadidifu ndani na nje ya nchi.

 

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. This best sativa edibles felt like a huge balanced option. It wasn’t too ample and didn’t needy too far-off in the other instructing either, which made it a expert pick pro new parts of the day. The flower looked премиум, nicely trimmed, and tranquil wholesome instead of dry and crumbly. The flavor came in all respects disinfected with a reduce sweet and abandoned note that made it enjoyable all the way through. Definitely a by-product that feels consistent and genially send down together.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button