DAR ES SALAAM; WANAWAKE 18300 wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali nchini wanatarajiwa kuwezeshwa kukua kibiashara na kuyafikia masoko makubwa kwa kupatiwa Msimbomilia (Barcodes).
Kampuni ya GS1 Tanzania imeandaa matembezi maalum (Barcodes Charity Walk) yanayotarajiwa kufanyika Septemba 15,2024 ili kuwezesha upatikanaji wa utambulisho huo.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi matembezi hayo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa maendeleo wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Sempeho Manongi amesema Msimbomilia ni muhimu katika kufikia soko la kimataifa.
“Serikali imejikita katika kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini na milango imefunguka kwa ukubwa mara baaada ya kusaini mikataba ya kibiashara, tunalo soko huru la Afrika, soko la Afrika Mashariki, soko la nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara (SADCC),”amesema
” Barcodes ndio utambulisho wa bidhaa kwenye ulimwengu wa kidijitali ambapo alama hiyo ukiiscan inaonesha kwamba nani ameizalisha, ni bidhaa gani na inamtambulisha mfanyabishara kwa mteja kwa kutumia njia rahisi ya manunuzi, hivyo ni vema muwe nazo ili kufaidika na masoko ya nje ya nchi,” ameongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa GS1Tanzania, Fatma Kange amesema kuwa digitali sio kutumia mitandao ya kijamii tuu bali na barcodes, ambayo gharama zake zimepunguzwa kutoka Sh 235.000 hadi kufikia Sh 75,000