Wanawake wajiamini uongozi- Mahela

NAIBUĀ Katibu Mkuu wa Afya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk Wilson Mahela amewataka wanawake kujiamini pindi wanapopewa mamlaka za kiuongozi kwani asilimia kubwa ya wanawake wakipewa uongozi hufanya vizuri.

Dk Mahela alisema hayo jijini Arusha wakati akifungua semina ya siku mbili ya watafiti wa mradi wa kuleta usawa wa kiuongozi katika mfumo na miundombinu kwenye sekta ya afya.

Alisema katika sekta ya afya ngazi ya chini asilimia 80 ya watumishi wa sekta hiyo ni wanawake lakini wengi wao sio majasili na wanashindwa kujiamini pindi wanapopewa madaraka hivyo baada ya semina hiyo anatarajia kuona wanawake watajitambua na kujiamini na hatimaye kupewa madaraka kwa kuwa ni waaminifu na waadilifu.

Naibu Katibu Mkuu alisema mradi huo unahamashisha wanawake kushika nafasi mbalimbali katika sekta ya afya kwa kuwa wengi wao ni watumishi katika sekta hiyo na Tamisemi inaunga mkono jitihada hizo na kuwataka wanawake kujitoa na kuwa wajasili na kujiamini katika shughuli za kiutendaji ili wawe viongozi bora baadaye.

Alisema wanawake wanauwezo wa kuongoza wakiwezeshwa na Tamisemi imeona hilo ni jambo jema kwa kuwajengea uwezo wanawake kushika nafasi mbalimbali katika sekta ya afya kwa kuwa wanajituma na hawasukumwi katika utendaji kazi wa kila siku katika sekta hiyo na serikalini

Dk Mahela alisema katika halmashauri kote nchi waganga wafawidhi katika vituo vya afya wengi wao ni wanawake lakini hawajiamini na kushika nafasi hizo kwa muda mrefu hivyo aliwataka wanawake kujiamini ili waweze kupanda ngazi za juu kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.

Alisema Rais aliyepo madarakani Rais Samia Suluhu Hassan ni mwanamke na toka aingie madarakani amekuwa akifanya vizuri katika sekta ya afya na serikalini kwa ujumla hivyo wanawake wanapaswa kuiga mfano wa Rais wao na kuondoka hapo walipo na kwenda kushika nafasi za juu katika sekta hiyo.

Naye mwanzilishi wa mradi huo,Professa Henry Mollel wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema mkakati wa Kitaifa ni kupata uwakilishi mzuri wa akina mama katika sekta ya afya kwani watendaji wakubwa katika sekta hiyo ni wanawake.

Professa Mollel alisema mradi huo unalenga katika kutekeleza malengo ya serikali ya kutaka wanawake waliojiendeleza kushika wadhifa mbalimbali serikali hususani sekta ya afya ambayo asilimia kubwa inaendeshwa na wanawake.

Alisema semina hiyo kwa kuanzia imeanza kwa kuwapa ujasili wa kiuongozi wanawake wa sekta ya afya wa Mikoa mitatu Kilimanjaro ,Kagera na Njombe lengo ni kufanya semina katika sekta hiyo kwa mikoa yote nchini.

Naye Msimamizi Mkuu wa Mradi Dk Anosisye Kasela alisema kuwa lengo kuu la mradi ni kutatua malengo yanayokwamisha wanawake kupata uongozi sekta ya afya na serikali hivyo semina hiyo inawapa udhoefu ili waweze kujiamini na kuwa wajasiri pindi wanapopata uongozi.

Dk Kasela alisema ana uhakika baada ya semina hiyo wanawake wengi watapata nafasi za kiuongozi katika sekta ya afya na kufanya vema kwani tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wakipigwa wanakuwa wazuri katika kuongoza.

Habari Zifananazo

Back to top button