Wanawake watakiwa kushiriki uchaguzi Mwanza

MWANZA: WANAWAKE jijini Mwanza wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kidemokrasia na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa ajili ya kuwachagua madini, wabunge na Rais wa nchi.

Hayo yamesemwa Juni 26 mwaka huu na Mwenyekiti wa Umoja wa Wake wa Viongozi wa Kitaifa, Tunu Pinda alipokuwa akizungumza katika hafla ya ugawaji wa nishati safi ya kupikia majiko 25 ya gesi ya kupikia kwa wanawake wanufaika wa TASAF.

Amesema majiko hayo yametolewa na umoja huo kama mchango wao wa kuunga juhudi za Tasaf katika kuwahidumia wananchi ambao hawana uwezo ili waweze kuyatumia kwenye shughuli zao za ujasiriamali kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

Mama Tunu Pinda akisakata dansi na watoto

Pinda ambaye pia ametembelea miundombinu ya kituo cha Fumagila,ambayo imepandishwa hadi na kuwa kituo cha afya aliupongeza uongozi wa TASAF makao makuu kwa uwekezaji mkubwa ilioufanya kwa kukamilisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, wagonjwa wa ndani na jengo la upasuaji.

Amesema wameridishwa na ujenzi wa majengo mazuri na yanatia moyo na kwamba umoja huo kuwa zahanati hiyo itakwenda kutoa huduma bora za afya kwa wakazi wa Fumagila ili waweze kushiriki vyema kwenye shughuli za uzalishaji mali.

Moja ya jengo zuri la wagonjwa wa ndani lililojengwa kwa ufadhili wa Tasaf katika kituo cha afya Fumagila katika wilaya ya Nyamagana.

Kaimu Mkurugenzi wa TASAF Desta Laiser amesema mbali na mambo mengine, utekelezaji wa miradi ya Tasaf umeboresha ujenzi wa ndoa imara katika ngazi ya familia

Amesema kituo hicho cha afya Fumagila kimejengwa kwa ushirikiano na wananchi kwa nia ya kuwawezesha kutambua kuwa ni kituo chao.

Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Dk Aman Kategele amesema zahanati ya Fumagila ilipandishwa hadhi kuwa kituo cha afya Februari 12 mwaka huu ambapo awali ilikuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 40 kwa siku ambapo kwa sasa kinahudumia wagonjwa 3000 kwa mwezi na watu 80 kwa siku.

Amesema ujenzi wa miundombinu mipya ya kituo hicho itasaidia kupunguza usumbufu kwa wananchi kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma za afya katika hospitali ya wilaya.

Amesema ujenzi wa miundombinu hiyo mipya imejengwa kwa gharama ya Sh milioni 452.70 na mchango wa wananchi wa Sh milioni 18.94.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button