Mradi wa Pamoja kunufaisha watu 41,000

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said, amesema jumla ya wanufaika 41,000 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wanatarajiwa kunufaika na Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia (PAMOJA) unaotekelezwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Balozi Zena amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi Zanzibar, Ziwani, akieleza kuwa mradi huo utatoa elimu na mafunzo ya uendeshaji bora wa biashara kwa wanufaika kabla ya kuanza kupatiwa mikopo kwa ajili ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi. SOMA: Wawekezaji Ufaransa Waalikwa Zanzibar

Amesema  mradi huo pia utasaidia kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na udhalilishaji, hususan kwa wanawake na watoto, kwa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa waathirika pamoja na kutoa huduma za ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia.

Aidha, amesema vituo vya malezi ya watoto wa awali vitajengwa na baadhi ya majengo kukarabatiwa ili kuwawezesha wazazi, hususan kina mama, kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji huku watoto wakilelewa katika mazingira salama.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Abeida Rashid Abdalla amesema mradi huo ni matokeo ya juhudi za viongozi wakuu wa nchi na unatekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano, huku mikopo itakayotolewa ikianzia shilingi 500,000 hadi milioni 30 na kurejeshwa ndani ya miezi 12 hadi 24.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. These carts near me thc felt like a de facto cordial mid-section ground. Nothing too inequitable, simply a level and balanced experience that worked well quest of casual use. The decorum was preferably than expected, and the texture was courteous a substitute alternatively of exceedingly gooey or tough. They also force gist as inclined gummies THC because the inclusive vibe felt easy, enjoyable, and illustrious into relaxing socially or scarcely hanging out. All from flavor to nature to consistency felt articulately done here.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button