Wanufaika wa mbolea Makete waanza kuvuna matokeo

MAKETE: Zaidi ya vijana 160 wa Wilaya ya Makete walionufaika na msaada wa mbolea bure kutoka kwa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea (TFRA) wameanza kufurahia matunda ya mtaji waliouomba kutoka serikalini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya vijana waliotembelewa na TFRA kuona maendeleo yao wamesema mtaji wa mbolea waaliopewa umeleta matokeo mazuri na kuacha alama isiyofutika.

Pia vijana hao wamekumbushana kuulinda mtaji kwa kuweka akiba ya pesa ya kununua mbolea baada ya mavuno ili kujiandaa na misimu inayofuta.

Mwishoni mwa mwaka jana 2025, ofisi ya mkuu wa wilaya ya makete iliwasilisha ombi kwa mamlaka ya udhibiti mbolea TFRA kwa niaba ya vijana zaidi ya 160, wakiomba msaada wapate mtaji ili kufanya kilimo chenye tija, ambapo uongozi wa TFRA chini ya Mkurugenzi Mtendaji Joel Laurent, ilipokea ombi hilo na kutekeleza kwa vitendo.




