Wami Dakawa waomba wasaidiwe kumalizia zahanati

WANANCHI wa Kijiji cha Wami Dakawa, mkoani Morogoro wamemuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo kuwasaidia ili fedha zipatikane kumalizia maboma ya Zahanati ya Dakawa, ambayo haijakamilika kwa zaidi ya miaka 10 .

Katibu wa Shina namba 18 la CCM katika Kijiji cha Wami Dakawa, Sixstus Lugenge alisema hayo jana wakati akisoma risala kwa kiongozi hiyo aliyefika kuangalia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya wananchi.

Lugenge amesema moja ya changamoto katika eneo lao ni kutokamilika kwa baadhi ya majengo ya zahanati hiyo tangu mwaka 2013, hivyo kufanya huduma nyingine kushindwa kutolewa katika kituo hicho cha afya.

“Tunaomba utusaidie ili kukamilisha maboma ya zahanati yetu ambayo tangu mwaka 2013 hayajakamilika,”amesema Lugenge.

Akizungumzia changamoto hiyo Chongolo amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mvomero,Philipina Titus kuhamisha matumizi ya fedha kwenye mafungu ili kuelekeza kiasi cha fedha kitumike kumalizia majengo hayo.

online pharmacy zoloft no prescription with best prices today in the USA

“Hili la maboma mkurugenzi fanya realocation (kuhamisha matumizi ya mafungu ya fedha),mwaka huu wa fedha ili majengo hayo yakamilike,na mimi nachangia shilingi milioni moja sasa hivi,”amesema Chongolo.

online pharmacy zantac no prescription with best prices today in the USA

Zahanati hiyo kwa sasa inatumia baadhi ya majengo yaliyokamilika kutoa huduma za tiba ikiwemo jengo la kujifungulia wajawazito na tiba kwa wagonjwa wa nje.

online pharmacy stromectol no prescription with best prices today in the USA

Habari Zifananazo

Back to top button