Wapania kumpeleka Baba Levo bungeni

KIGOMA: NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Taifa Kilumbe Ng’enda amesema wamejiandaa kuhakikisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia CCM, Clayton Chipando maarufu ‘Baba Levo’ anaingia bungeni katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.

Ng’enda amesema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa chama hicho mkoani Kigoma alipowasili kwa mapumziko mafupi baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya wazazi CCM Taifa.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa chama kimeamua kumpitisha Baba Levo hivyo ni lazima viongozi na wanachama wote kuheshimu uamuzi huo lakini kumuunga mkono mgombea huyo ambaye kwa sasa anapambana na Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Pamoja na kusimamia kura za Baba Levo, Ng’enda amesema watahakikisha wanasimaamia kura za mgombea uraisi wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan, wabunge wote wa mkoa huo na madiwani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button