Wapewa elimu athari dawa za kulevya

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu juu ya athari za dawa za kulevya kwa wadau na taasisi zinazofanya kazi na vijana Jijini Arusha.

Elimu hiyo imetolewa na Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka DCEA, Sarah Ndaba pamoja na viongozi wengine wa mamlaka hiyo na kushirikisha wadau 152 kutoka taasisi/asasi mbalimbali kikao hiko kilichokuwa na lengo la kujadili sera ya vijana iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Baada ya washiriki hao kupata elimu, akiwemo Jumanne Mohamed wameahidi watafikisha ujumbe huo kwa vijana kama sehemu yao ya kushiriki katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya mkoani Arusha.

SOMA: DCEA yakamata dawa za kulevya kilo 3182

Habari Zifananazo

Back to top button