Wapewa elimu athari matumizi dawa za kulevya

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga kwa waumini wa dini ya kikristo zaidi ya 250 katika Kanisa la Kikatoliki Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga USA River katika Wilaya ya Arumeru mkoani wa Arusha.

Elimu hiyo imetolewa leo na Ofisa Elimu Jamii wa DCEA Kanda ya Kaskazini,Shabani Miraji ambapo alieleza dhamira ya mamlaka ya kutoa elimu hiyo katika nyumba za ibada za imani mbalimbali katika mikoa yote ya Kanda ya Kaskazini.

SOMA: DCEA yakamata dawa za kulevya kilo 3182

Waumini walioshiriki ibada kanisani hapo waliaswa kutojihusisha na biashara pamoja na matumizi ya dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao za mafanikio ya baadaye lakini pia walihimizwa juu ya kutowabagua waraibu wa dawa hizo na badala yake wawaunganishe katika vituo vya huduma za matibabu zilizopo karibu na mazingira yao wanayoishi.

Amesema ofisi ya Kanda ya Kaskazini ya Mamlaka ya Kdhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii zikiwemo nyumba za ibada za imani zote ili kuhakikisha kila kundi linafikiwa katika maeneo yote ya Kanda ya Kaskazini.

Habari Zifananazo

Back to top button