Wapewa mwongozo kuwasaidia wananchi msaada wa kisheria

TIMU ya wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushiriana na waratibu wa kampein ya msaada wa  kisheria  ya Mama Samia wametoa mafunzo ya mwongozo wa kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera watakaojitokeza kuwasilisha changamoto zao za msaada wa kisheria.

Wataalamu walionufaika na mafunzo ya mwongozo na maofisa ustawi wa jamii, maofisa naendeleo ya jamii, maofisa ardhi, mawakili wa kujitegemea, maofisa wa jamii kutoka kwenye madawati ya polisi ,watakaokuwa kwenye kampeini hiyo, watendaji wa kata zitakazotembelewa, wanasheria kutoka ngazi za halmashauri  zote za Mkoa wa Kagera.

Advertisement

Mkurugenzi wa Kampeini ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (MSLAC) Ester Msambazi  akizungumza amesema anajivuni kuanzishwa kwa kampeini hiyo kwani kuna mafanikio makubwa  sana  tangu ilipoanzishwa Mei 2023 ikiwa ni pamoja na utatuzi wa migogoro na kesi zilizodumu muda mrefu pamoja na wananchi kupata elimu ya namna bora ya kuwasiliana na mawakili ili kufungua kesi zao.

“Tunapotoka hapa baada ya kupatiwa mafunzo ya miongozo ni lazima tuvue vyeo vyetu vyote,tuviweke pembeni tuwe kitu kimoja tufanye kazi kwa weledi tuwe wasikivu, lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata msaada wa kutosha na kampein hii inafanikiwa kufufua  matumaini ya wananchi wanyonge ,kwa sababu wananchi wengi wanaokumbwa na changamoto  hawana uwezo,”amesema  Msambazi.

Amesema kampeini ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inatarajia kutamatika Mei mwishoni mwaka huu na mara baada ya kampein hiyo kliniki za kutoa huduma za kisheria bure kila halmashauri zitafunguliwa na wananchi wanaendelea kupata huduma huku mwananchi ambaye kesi yake haitapata utatuzi kwa siku 9 atapewa Wakili wa kumusimamia mpaka kesi yake imalizike.

Kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Issaya Tendega amesema Mkoa wa Kagera unakumbwa na matatizo makubwa  na inahitaji msaada wa kisheria katika nyanga ya migogoro ya ardhi,mirathi na unyanyasi wa kijinsia

Aidha ametoa wito kuhakikisha wananchi wanaoishi vijijin vya pembezoni kupata msaada wa kisheria kwani mara nyingi hawana nauli na gharama za kugharamikia kesi zao.

“Kama mkoa wa Kagera tutafurahi Kuona wananchi wetu migogoro inapungua  kupitia changamoto kupitia kampeini hii, baadhi ya wananchi wanaogopa kusajili kesi zao waliogopa gharama hivyo uwepo wa kampeini hii ni fursa kwa wananchi  wote ,hivyo timu zilizopangwa zifanye kazi kwa weledi “amesema Tendega.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *