Wapinzani wasifu kuimarika demokrasia miaka minne

Mwenyekiti wa Chama cha AdaTadea na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib.

WADAU wa siasa wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuimarisha demokrasia.

Mwenyekiti wa Chama cha AdaTadea na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania, Juma Ali Khatib amesema katika miaka minne ya uongozi wa rais Samia, demokraisa imeimarika.

Khatib alilieleza HabariLEO kabla ya Rais Samia vyama vya siasa vilikuwa vina hali ngumu kutokana na katazo la kufanya mikutano ya hadhara lakini sasa hali ni tofauti.

Advertisement

Alisema pia serikali imeliboresha baraza hilo kwa kulitengea fedha kuliwezesha lifanye shughuli zake.

“Sasa hivi tuna bajeti hivi karibuni Machi 11 hadi 13 Baraza la Vyama vya Siasa na wajumbe wa vyama mbalimbali tulikuwa mkoani Morogoro katika mkutano, sasa hivi tunaweza kufanya vitu vingi tofauti na awali,” alisema.

Ameiomba serikali itoe ruzuku sawa kwa vyama vyote vya siasa ili visivyo na uwezo vifike kwa wananchi kunadi sera zao.

“Inabidi tuzunguke nchi nzima lakini kuna baadhi ya vyama havina uwezo wa kufanya hivyo, mfano mimi nataka kugombea urais Zanzibar na mwenzangu atagombea bara tupewe uwezo wa kuzunguka kote ili uchaguzi ukiisha tusema tumepambana wote lakini wananchi wamekuchagua wewe,” alisema Khatib.

Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mkoa wa Mwanza, Iddi Kiula alisema falsafa ya Rais Samia ya 4R (maridhiano, ustahimilivu, mageuzi na kujenga upaya) imepunguza vikwazo katika demokrasia.

Ameiomba Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) isimamie sheria katika uchaguzi mkuu ujao baadaye mwaka huu kwa kuzingatia haki na weledi na iwatangaze watakaoshinda kihalali.

“Rutuba ya demokrasia ni haki, haki itendeke kwa kuhakikisha kuwa tunalolifanya lina maslahi kwa wote kwa kufanya hivyo nchi itaendelea kujengeka,” alisema Kiula.

Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Richard Lyimo alisema demokrasia nchini imeimarika ikilinganishwa na awali.

Alisema Rais Samia amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kurejesha ruhusa ya vyama vya siasa kufanya mikutano.

Lyimo alisema ili kuimarisha demokrasia iliyopo ni muhimu serikali iifanyie kazi hoja ya vyama vya upinzani ya Katiba mpya.

“Baada ya uchaguzi nafikiri ni muda mzuri wa kulifanyia kazi suala hilo, wengi wanalalamika lakini naamini Rais Samia atalifanyia kazi maana ni msikivu,” alisema.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Richard Feruzi alisema falsafa ya 4R imeimarisha demokrasia nchini.

“Baada ya kuingia madarakani kupitia maridhiano tumeona viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ambao walikuwa nje wakirejea nchini mfano Tundu Lissu, Lema na Wenje hii ni ishara ya demokrasia kurudi nchini,” alisema.

1 comments
  1. Can you imagine making $18,000 a month while working from home just a few hours a day? I’m doing it, and I never thought it was possible until I found this online opportunity. The work is super easy, and you don’t need any prior experience—just a desire to succeed! I can’t believe how much my life has changed in such a short time. If you’re ready to take control of your income, visit the website and get started today!

    Visit This…… W­w­w­.­E­a­r­n­A­p­p­1­.­C­o­m

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *