Warembo 13 kuwania Miss Ilala 2026

DAR ES SALAAM: Warembo 13 wanatarajiwa kushindana katika fainali za Miss Ilala 2026, zitakazofanyika Oktoba 24, mwaka huu, katika Ukumbi wa The Dreamer’s Lounge, Chanika, Dar es Salaam, huku washindi watano wa kwanza wakitarajiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha wilaya hiyo katika shindano la Miss Tanzania 2026.

Uzinduzi wa shindano hilo ulifanyika jana Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam, ambapo waandaaji walieleza kuwa maandalizi yamekamilika, ambapo Mkurugenzi wa Shindano la Miss Tanzania 2026, Diana Rutainurwa, amesema wamejipanga kuhakikisha msimu huu Miss Ilala inakuwa ya kipekee.

Amesema warembo wote 13 wanaoshiriki shindano hilo wana sifa zinazohitajika, huku akieleza kuwa wana matumaini washindi watano wa kwanza wataiwakilisha Ilala vizuri katika shindano la Miss Tanzania.

Ameongeza kuwa fainali hizo zitapambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali, hatua inayotarajiwa kuongeza mvuto kwa mashabiki na wadau watakaohudhuria tukio hilo.

Diana ameomba ushirikiano kutoka kwa viongozi wa Wilaya ya Ilala pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa mafanikio na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button