Wasakwa kwa kuiba $6.2m kutumia sahihi ya rais mstaafu Nigeria
NIGERIA inahitaji usaidizi wa Shirika la Polisi la Kimataifa la Uhalifu (nterpol) ili kuwakamata washukiwa watatu wanaodaiwa kuiba $6.2m kutoka benki kuu, kwa kutumia sahihi ya kughushi ya Rais mstaafu Muhammadu Buhari.
Mamlaka zinaamini kuwa washukiwa hao walikula njama na aliyekuwa mkuu wa benki kuu ya Nigeria Godwin Emefiele.
Tayari anakabiliwa na mashtaka 20, ikiwa ni pamoja na kupokea $6.2m kinyume cha sheria.
Emefiele amekana mashtaka yote, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana.
Waendesha mashtaka pia wanadai kuwa Emefiele aliidhinisha kinyume cha sheria kutolewa kwa pesa hizo kutoka kwa hazina ya benki kuu.
Katika taarifa yake Desemba mwaka jana, alitaja madai hayo kuwa “uongo mtupu uliosemwa na mpelelezi ili kufanikisha ajenda yake ya kishetani”. Alitoa wito wa “uchunguzi wa kina na wa uwazi”.