Wasanii waitwa kwenye mafunzo Dar

WASANII wa tasnia mbalimbali watashiriki mafunzo yatakayowasaidia kuendeshea kazi zao, katika Tamasha la Kimataifa la Maendeleo ya Filamu na Sanaa Tanzania lililoandaliwa na Bodi ya Filamu Tanzania.
Mafunzo hayo yatafanyika Desemba 11 hadi 15 katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia tamasha hilo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu, Gervas Kasiga amesema tamasha hilo linatarajiwa kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Hamisi Mwijuma ‘Mwana FA’

“Sio kwa wasanii wa filamu peke yao hata wasanii wa Bongo Fleva na sanaa mbalimbali wajitokeze na kujifunza kwa yanayofundishwa katika tamasha hili ikiwa ni kufanya kazi bora za sanaa kuangalia masoko na kutangaza kazi kitaifa na kimataifa,” amesema.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko upande wa mikopo, Nyakao Mturi Nyaemba amesema mikopo tunayotoa kwa wasanii itasaidia kuendeleza kazi zao za sanaa lakini kupitia tamasha hili watapata nafasi ya kupewa mafunzo ya ufanyaji kazi na kunifaika na mikopo wanayopewa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Cosota Doreen Sinare amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wasanii jinsi ya kujisajili na kusajili kazi zao ili kukusa na kulinda kazi zao.

Habari Zifananazo

Back to top button