“Wasanii wazingatie mila, desturi”
WASANII wa muziki nchini wameshauriwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili, mila na desturi.
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Kedmon Mapana ametoa kauli hiyo Agosti 23 alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
Dk Mapana amesema wasanii wanatakiwa kufanya sanaa kwa kufuata mila na desturi huku wakiwa mabalozi wazuri katika kueneza na kudumisha utamaduni wa nchi yetu ya Tanzania.
“Wanatakiwa kuangalia na kuzingatia mila zetu zipoje wanapoandaa kazi zao na kujua zina manufaa gani kwenye jamii mara baada ya kusikiliza nyimbo zao,itasaidia kulinda mila na tamaduni zetu.
“Unapofanya kazi unatakiwa kuangalia ina manufaa gani kwenye jami. Unatakiwa kwa makini kabla ya kuiachia katika mitandao, unapaswa kufuata tamaduni zetu,” amesema Dk Mapana.
View this post on Instagram