Washiriki ‘Samia Bonanza’ waomba vifaa vya kisasa

WASHIRIKI wa michezo mbalimbali ya ‘Samia Jumbe Holiday Bonanza’ Manispaa ya Shinyanga wamejitokeza kwa wingi huku wakiomba upatikanaji wa vifaa vya kisasa ili kukuza vipaji vyao.
Washiriki wa mbio za baiskeli wanaume na wanawake wametoa ombi hilo leo baada ya kuzinduliwa kwa bonanza hilo na Mratibu wa Michezo, Jackline Isaro katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga katika kusherekea siku ya mwaka mpya.
Jackline Isaro amesema michezo imefanyika huku akiwaomba majaji walioteuliwa kutoa uamuzi kwenye michezo mbalimbali watende haki.
Isaro amesema zitaanza mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake, ‘pool table’ na bao huku ukifuatiwa na mchezo wa mpira wa migu majira ya saa sita mchana kati ya timu ya bodaboda na bajaji na usiku utafanyika mchezo wa basketball.