Wasiofuata sheria washughulikiwe – Kihenzile
KAMATI ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira imeitaka Serikali kuvichukulia hatua za kisheria Viwanda vyote vinavyotekeleza shughuli zake bila kufuata taratibu za kimazingira.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo David Kihenzile mara baada ya ziara ya kamati hiyo kukitembelea kiwanda kinachozalisha dawa mbalimbali za binadamu cha Shelly Pharmaceutical kilichopo Mwenge.
Akiwa kiwandani hapo pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, akiwemo Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Raise Muungano na Mazingira KhamisKhamis Hamza Khamis, Kihenzile amesema lengo la hatua hiyo pamoja na mambo mengine ni kulinda afya za wananchi pamoja na viumbe hai.
“Tunapongeza utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika kiwanda hiki, ukweli wanafanya kazi nzuri kwa kuyaweka mazingira katika hali ya usafi kuanzia uhifadhi taka hadi mifumo ya maji ya viwandani, huu ni mfano wa kuigwa” amesema Kihenzile
Amesema suala la kutunza mazingira hasa kwa maeneo ya viwanda ni muhimu kwa kuwa litasaidia kulinda afya za wananchi wa maeneo ya karibu badala ya kuwasababishia maradhi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Viwanda ameitaka Ofisi hiyo ya Makamu wa Rais Mazingira kutoa elimu kwa wananchi juu ya utengenishaji wa taka ili kutoa urahisi kwa wasafirishaji wa taka hizo kwenda dampo.
Kwa upande wake Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Raise Mazingira Khamis Hamza Khamis alisema wao kama Serikali watahakikisha suala la ukaguzi katika maeneo ya viwanda wanalipa umuhimu ili kulinda aina yoyote ya uhalibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza.