Wasira aahidi kuendeleza maridhiano

DODOMA;MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema chama hicho kinataka dunia itambue kuwa ni cha amani na maendeleo, ndiyo ajenda kuu hivyo kitaendeleza maridhiano na jamii na si mtu mmoja.

Kauli hiyo aliitoa jana Dodoma baada ya kucha guliwa na Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara .katika uchaguzi uliofanywa na kuibuka mshinda kwa kura 1,910 kati ya kura 1,917 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano.

Uchaguzi huo umekuja ili kumpata mrithi wa nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Ab dulrahman Kinana aliyean dika barua ya kujiuzulu wad hifa wake kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan Julai 29, mwaka 2024 na Kamati Kuu kuridhia ombi hilo.

Wasira alishukuru kamati na wajumbe wote kwa kupata heshima hiyo na kusema Mungu hutumia watu kupata watu na kusema dunia itambue CCM ni chama cha amani na ajenga yao ni maendeleo.

“Nataka dunia ijue chama chetu ni cha amani, maendeleo ndiyo ajenda zetu, tunapewa nchi tufanye maendeleo lakini huwezi kufanya bila amani, sasa mwenyekiti wetu ana falsafa ya 4R na sisi tunaitekeleza,” alisema Wasira.

“4R zina maana ya Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya. Alisema katika hilo, CCM itaendeleza maridhiano na jamii na si mtu mmoja na kuwa jamii hiyo ni pamoja na viongozi wa dini, mashirika ya kijamii na wanajamii wote. “

“Kama wewe una chama chako kinataka vita tutakuambia huku hatuendi, tunataka amani,” alisema Wasira.

Alisema kwa sasa anaanza na mambo mawili ambayo ni kazi za chama hicho ambazo ziko ndani ya Ibara ya tano ya Katiba ya CCM.

“Kazi ya chama hiki iko ibara ya tano ya chama chetu, kushinda uchaguzi, kushika dola, mengine yote yanafuata, sasa uchaguzi wa serikali za mitaa tayari, tumeshinda kwa kishindo, kazi tuliyo nayo ni kuka mata dola Bara (Tanzania) na Zanzibar kwa kura,” alisema Wasira.

Alisema hilo linaweze kana kwani chama kime tekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi na mifano halisi inaonekana.

Alitoa mfano wa ujenzi wa shule, miradi ya maendeleo na huduma nyingine za jamii. “Miradi mingi inakami lika, sasa tushindwe kwa sababu gani? Sababu za kushinda tunazo, nia ipo na uwezo tunao, twendeni tukashinde,” alisema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button