Wataalamu Vyuo Vikuu wahusishwa Sensa

MTAKWIMU  Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa, amesema matokeo ya Sensa yanayotangazwa leo Oktoba 31,2022 yamefanyiwa kazi kitaalamu kwa asilimia 98 yakihusisha wataalamu kutoka Vyuo Vikuu na wataalamu kutoka sehemu mbali mbali.

Akitoa salamu zake wakati wa uzinduzi wa matokeo ya mwanzo ya Sensa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Chuwa amesema ili kutoa matokeo sahihi pia serikali imeshirikiana na Shirika la Marekani kitengo cha Sensa pia Kamisheni ya Sensa ya uchumi ya Umoja wa Mataifa.

Amesema kazi iliyofanyika inaenda sanjari na matakwa ya Umoja wa Mataifa.

“Kwa mujibu wa sheria ya takwimu ya 351 sura ya 51, sasa tutakuwa na idadi kamili ya watu wetu, takwimu hizi zitatumika kupanga maendeleo ya nchi yetu.” Amesema Chuwa na kuongeza

“Muheshiwa Rais, muongozo utakaozindua muda mfupi ujao, hili ufanikiwe sawa sawa na kuleta tija, tutatoa mafunzo ya kutosha katika ngazi zote za utawala kuanzia juu mpaka chini kwa ajili ya kupanga maendeleo yao.”Amesema Chuwa

Amesema pia kupitia Sensa ofisi yake ina takwimu zote za wafanyabiashara ndogo ndogo, hivyo kwa sasa taasisi za kifedha ikiwemo mabenki wanaweza kuwapatia mikopo wafanyabiashara hao bila kulazimika kuwasilisha hati za viwanja.

Chuwa amesema kazi kubwa iliyopo hivi sasa ni kufanya uchambuzi wa kina wa makazi ya watu na wanavyoishi watu na maisha yao.

Habari Zifananazo

Back to top button