SHEKHE wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Kiburwa amewataka waumini wa dini zote nchini kufuata matendo na mienendo mema ya mitume ili kuwezesha watu kuishi kwa amani na upendo na kuondokana na vitendo viovu ikiwemo utekaji.
Shekhe Kiburwa ametoa kauli hiyo katika Baraza la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) ambalo kimkoa lilifanyika mjini Kigoma likitanguliwa na mkesha wa Maulid.
SOMA: Serikali, viongozi wa dini kushirikiana
Shekhe wa Mkoa Kigoma na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Taifa (BAKWATA) Hassan Kiburwa akizungumza katika baraza la maulid ya kumswalia Mtume Muhamad (S.A.W) lililofanyika mjini Kigoma
Shekhe huyo amesema mafundisho ya vitabu vya dini zote ikiwemo Qur’an na Biblia vinaelezea namna waumini wa dini hizo wanapaswa kufuata matendo mema ya mitume na namna ya kuwafanya waishi kama ndugu kwa upendo na amani jambo ambalo linasaidia kuondoa matendo yasiyofaa.
Mkurugenzi wa Shirika la African Relief Organisation Kigoma, Salahudeen Abdul Wahab alisema kuwa dini izote zimekuwa zikitoa mafundisho ya kuishi katika maadili mema yenye upendo hivyo amewataka watu wote kurudia mafundisho ya dini zao kuondokana na matukio maovu na ya ukatili yanayotokea nchini.
Mkurugenzi wa Shirika la African Relief Organisation Kigoma, Salahudeen Abdul Wahab (kushoto aliyesimama) akizungumza katika Baraza la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W) lililofanyika mjini Kigoma
SOMA:Serikali inathamini mchango wa madhehebu ya dini
Viongozi na waumin wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria Baraza la Maulid mkoani Kigoma
Mwalim Rashid Juma kutoka Bakwata mkoa Kigoma akizungumza katika baraza hilo la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (SAW) amewasihi Waislam na wasio waislam nchini kukataa kutumika katika matendo maovu yanayopelekea kuondoa uhai wa watu na kuvunja amani ya nchi hivyo kutaka kila mmoja kupiga kelele kusitishwa kwa vitendo hivyo.