Watakiwa kusajili bidhaa zao

ARUSHA; WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), amewataka wavumbuzi wa vifaa,dawa na bidhaa nyingine kuhakikisha wanasajili bidhaa zao kabla hawajaanza kuzitumia ili kuepuka kushtakiwa kwa kuvunja sheria za nchi.

Akitoa elimu  kwa wafanyabiashara jijini Arusha, Msajili Msaidizi wa BRELA, Benedictson Byamanyilwowa,  amesema  wakala wameamua kutoa elimu maeneo mbalimbali nchini  ikiwemo wafanyabiashara ili kuwaepusha na usumbufu wa kisheria.

Amesema kwa sasa teknolojia na uvumbuzi vimekuja kwa kasi, hivyo wapo baadhi ya watu wanavumbua vifaa mbalimbali vinavyotatua matatizo mengi katika jamii na kuanza kuvitumia sokoni  au katika jamii bila kusajili BRELA.

“Hata wale wavumbuzi wa vyuo vikuu vya kati wapo wanaovumbua vifaa vyao, ni lazima wote kabla hawajaanza kupeleka sokoni au katika jamii wakilete kwetu kusajili na wapo hata baadhi yao wanapeleka katika maonesho ya Sabasaba au Nanenane kabla hawajasajili hili ni kosa,” amesema.

Naye Ofisa Msajili BRELA, Julieth Kiwelu amesema  wakala hao wanatoa elimu  kwa ajili ya kuongezea uwezo wafanyabiashara, ili watumie bunifu zao katika biashara zao.

Ofisa  Biashara wa Chama cha Wafanyabishara Mkoa wa Arusha,Charles Makoi alishukuru BRELA kwa kutoa elimu hiyo ambayo itawasaidia kufanyabiashara kwa kufuata sheria na kuepuka ufanyaji biashara kimazoea.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button