KAMPUNI kubwa za kimataifa za kilimo cha bustani hupata matatizo kupata wafanyakazi waliofunzwa vyema katika sekta hiyo hapa nchini, hali inayosababisha kuajiri wafanyakazi kutoka nchi nyingine na kuwalipa mishahara mikubwa.
Akizungumza na wakuu wa vyuo mbalimbali vinavyojihusisha na kilimo jijini Arusha, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe de Boer, amesema katika kuziba pengo hilo, baadhi ya kampuni zimeanzisha programu zao za mafunzo ya kilimo cha bustani, ili kuwasaidia wahitimu wanaotoka vyuo vya kilimo kupata maarifa zaidi na kujiajiri.
Amesema baadhi ya kampuni za kilimo huajiri watu kutoka nje ya nchi kutokana na waliopo kukosa sifa, hivyo ubalozi huo kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali Kanda ya Kaskazini wanashirikiana kutoa elimu juu ya kilimo na aina gani ya kilimo kinachotakiwa na wamiliki wa mashamba mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Alisema programu hiyo inayotolewa na ubalozi huo imeshirikisha Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC) na Chuo cha Kilimo cha Tengeru kwa kipindi cha miaka miwili