Watambulisha mvumo mpya upokeaji kazi

KAMPUNI ya Azam Media imetambulisha mfumo mpya wa upokeaji wa kazi za Sanaa za kitanzania zitakazoruka kwenye Chaneli ya Sinema Zetu kuepuka wizi wa kazi za Sanaa.

Akizungumza na habari leo, jijini Dar es Salaam, msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya amesema kuwa uzalishaji wa tamthia hiyo umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Siphia.

Amesema awalinilikuwa unapeleka demo kwanza kwa sasa hali imekuwa nitofauti unatakiwa kuingia mtandaoni kujisajili na kujaza fomu na kuweka mikataba mbalimbali ikiwemo mwandishi wa stori vibali vya Cosota.

Ameongeza kuwa waandaaji wapya wanaongia na kazi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Sophia.

Habari Zifananazo

Back to top button