Watano wauawa tukio la kufyatua risasi Somalia

TAKRIBANI watu watano, wakiwemo maofisa wa kijeshi wa Somalia na mwanajeshi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, wameuawa leo baada ya mwanajeshi mmoja kufyatua risasi katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu Mogadishu, ofisa wa jeshi na wafanyakazi wa hospitali wamesema.

Wizara ya ulinzi ya UAE ilisema wanajeshi wake watatu na ofisa mmoja wa Bahrain waliuawa katika tukio hilo walilooita kitendo cha kigaidi  nchini Somalia walipokuwa wakitoa mafunzo kwa wanajeshi wa Somalia.

Wengine wawili walijeruhiwa, wizara iliongeza.

Advertisement

Wizara haikutoa maelezo mengine kuhusu shambulio hilo lakini ilisema UAE “inaendelea kuratibu na kushirikiana na serikali ya Somalia katika kuchunguza  tukio hicho.

Mwanajeshi mpya wa Somalia aliyepata mafunzo, pia aliuawa kwa kupigwa risasi katika kituo cha kijeshi cha Gordon. “Askari huyo aliwafyatulia risasi wakufunzi wa UAE na maofisa wa kijeshi wa Somalia walipoanza kusali,” ofisa huyo wa kijeshi alisema.