OFISA leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Koyan Aboubakar amesema watu wengi hawana utamaduni wa kufuatilia taarifa za usajili kupitia mitandao yao hali inayofanya kutumia watu ambapo hutoa gharama kubwa au kutapeliwa wakati mwingine.
Akizungumza katika maonesho ya utalii yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yajulikanayo kama Swahili Export site, Koyan amesema kupitia maonesho hayo wanatoa elimu kwa wananchi ya namna ya kupata huduma na kutatua changamoto mbalimbali.
“Elimu kwa wafanyabisha bado ni changamoto huduma zetu zinapatikana kwenye mitandao na kwa watanzani wengi kutumia mtandao ni shida huwa wanatumia watu ambao wanarahisisha biashara zao wengine wanatapeliwa au kutoa gharama kubwa sana kupata huduma,”ameeleza.
Amesema wanapopata nafasi kama za maonesho ni rahisi kupata elimu na kupata huduma.
“Tumekuja kwenye maonesho ya site kwaajili ya kukutana na wafanyabishara wa sekta ya utalii na wengine na pia tunajua biashara yoyote lazima brela kama wakala wa serikali mwenye dhamana wakutane nao kwasababu ni wateja wakuu.
Aidha amebainisha kuwa katika maonesho hayo wafanyabishara wapya wamejisajili na wengine wenye changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kupatiwa uvumbuzi wamepata huduma.
“Tunatoa leseni za biashara, tunasajili makampuni na biashara, tunsajili alama za biashara na huduma za kutatua changamoto zilizojitokeza na hapa wateja wengi walikuwa na changamoto za kusajili majina ya biashara, kuhuisha taarifa za makampuni ,leseni za biashara na tunaendeleo kutoa huduma,”amesisitiza.
Amesema hawana kesi kubwa za usajili na leseni lakini wanataka kufikia wateja wao kwa wakati wanapowahitaji na wanafika kuwaelisha huduma wanazotoa na kutatua changamoto zilizopo.