DAR ES SALAAM: Watanzania wametakiwa kuzingatia matumizi bora ya umeme ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaondokana na matumizi yasiyokuwa ya lazima, kuwa na miundombinu bora ili kupunguza upotevu wa umeme.
Hatua hiyo itapunguza matumizi mabovu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 14 ya umeme unapotea kutokana na sababu hizo.
Hayo yamesemwa leo Novemba 5, 2024 na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Innocent Luoga wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam kuhusu Kongamano la Kikanda la Matumizi Bora ya Nishati lililoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) litakalofanyika Arusha Disemba 4 hadi 5,2024.
Meneja Mipango wa Umoja wa Ulaya Massimiliano Pedretti amesema Umoja wa Ulaya unafurahi kuona matokeo miradi inatekelezwa kwa viwango na kwamba wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuongeza muda wa utekelezaji na wataendelea kufadhiri masomo kwa wanafunzi mbalimbali ili kuwajengea uwezo kuhusu mpango huo.
Mtaalamu wa Mipango kutoka UNDP, Abbas Kitogo amesema katika kongamano hilo litakalohusu wadau mbalimbali watengeneza mkakati mzuri wa matumizi ya nishati hiyo, kuwa na rebo za vifaa, kuwa na mifumo mizuri ya matumizi, kujenga uelewa na kulinda .
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo linalotarajia kuwa na washiriki zaidi ya 400 mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Waziri Mkuu Dk. Dotto Biteko.