Watu 10 wameuawa kimakosa Nigeria

NIGERIA : WATU wapatao 10 wameuawa kimakosa wakati ndege ya jeshi la Nigeria iliyokuwa inawafuatilia majambazi katika vijiji viwili ilipowashambulia katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

Gavana wa jimbo hilo Ahmed Aliyu amesema raia wengine kadhaa walijeruhiwa kwenye shambulioa hilo.

Amesema ieshi lilikuwa na dhamira ya kupambana na makundi ya wahalifu wenye silaha lakini waliwapiga mabomu kimakosa watu wasio na hatia. SOMA: Watu 140 wageuka majivu Nigeria

Gavana huyo ameongeza kuwa serikali itashirikiana na mamlaka zingine kuchunguza operesheni ya kijeshi iliyosababisha vifo vya watu kwenye vijiji viwili vya Gidan Sama na Rintuwa kwenye jmbo hilo la Sokoto la magharibi mwa Nigeria.

 

Habari Zifananazo

Back to top button