NIGERIA : ZAIDI ya watu 140 wakiwemo watoto wamefariki dunia nchini Nigeria baada ya lori la kusafirisha mafuta ya petroli kupinduka na kusababisha maafa makubwa.
Kwa mujibu wa vikosi vya uokoaji nchini humo vimeeleza kuwa watu hao wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa ni kutokana na kukimbilia kuchota mafuta.
Mkuu wa huduma za uokoaji Dokta Haruna Mairiga amesema idadi kubwa ya miili imeharibika na kugeuka majivu kwa hiyo wamepanga kuwazika katika kaburi la halaiki katika eneo hilo.
Nigeria ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika na haina mfumo mzuri wa reli wa kusafirisha bidhaa za mafuta.
SOMA : Watu 17 wapoteza maisha ajali ya lori Nigeria