CONGO : WATU 10 wameuawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wenye itikadi kali wenye mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu (IS).
Waasi hao wa ADF walishambulia jana kijiji cha Makoko katika eneo la Lubero, Jimbo la Kivu Kaskazini.
Wakati wa mashambulizi hayo, hakukuwa na askari wa Congo katika kijiji hicho, ispokuwa wapiganaji wanaojulikana kama Wazalendo, ambao mara kadhaa wamekua wakishirikiana na vikosi vya Congo.
Hayo yameelezwa na mbunge wa jimbo hilo David Sikuli, ambaye ameitolea wito serikali ya Congo kuruhusu kutanuliwa kwa operesheni za pamoja Jeshi la Congo na Uganda hadi kwenye maeneo yote wanakopatikana waasi hao wa ADF.
Eneo la Mashariki mwa Congo linakabiliwa kwa miongo kadhaa na ghasia za makundi yenye silaha.
SOMA: DR CONGO : ADF yaua watu 12 Congo
Zaidi ya vikundi 120 vinapigania ushawishi, ardhi na rasilimali muhimu za madini, huku makundi mengine yakijaribu kutetea jamii zao.Ghasia hizo zimesababisha karibu watu milioni 7 kuyakimbia makazi yao.