Watu 11 wauawa shambulio la Urusi, nchini Ukraine

SHAMBULIO la kombora la Urusi limeua watu 11, wakiwemo watoto watano, Mashariki mwa Ukraine, Ofisa wa eneo hilo anasema.

Makombora ya S-300 yalipiga mji wa Pokrovsk katika eneo linaloshikiliwa na Ukraine Mkoa wa Donetsk, gavana wa eneo hilo alisema.

“Adui anapiga raia kwa dharau, akijaribu kuleta ghasia nyingi,” Gavana Vadim Filashkin alichapisha kwenye Telegram.

Advertisement

Katika hotuba yake ya jana jioni Rais Volodymyr Zelensky alisema vikosi vya Urusi vililenga maeneo yenye makazi ya watu.

Urusi inapaswa kuhisi matokeo ya mashambulizi kama haya hayafai.” Zelensky aliongeza.

Urusi haijatoa kauli yoyote kuhusu tuhuma hizo.

Pokrovsk iko karibu kilomita 70 (maili 43) Kaskazini-Magharibi mwa jiji la Donetsk, ambalo linakaliwa na vikosi vya Urusi.

Kabla ya vita ilikuwa na idadi ya watu wapatao 60,000. Baadhi ya wakazi wamekuwa wakirejea licha ya onyo rasmi kuhusu hatari hiyo.