SUDAN: WATU 127 wameuawa nchini Sudan kufuatia mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF.
Karibu watu 60 wameuawa katika mji wa Omdurman huku wengine zaidi ya 100 wakiuawa katika soko la Kaskazini mwa mji wa Kabkabiya huko Darfur.
Gavana wa Khartoum, Ahmed Othman Hamza, amesema kombora lililorushwa na RSF lilipiga basi la abiria na kuwaua watu wote 22 waliokuwamo ndani. SOMA: Sudan bado mtihani – Schulze
Pande hizo mbili ambazo zimekuwa zikipambana tangu Aprili mwaka 2023, zimeshutumiwa kushambuliana vikali kwa makombora na kuyalenga maeneo ya raia yanayokaliwa na watu wengi.