Watu 18 wafa wakigombea treni India

INDIA: TAKRIBAN watu 18 wamefariki na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kwenye kituo cha reli cha New Delhi nchini India baada ya kutokea mkanyagano uliosababishwa na idadi kubwa ya watu.

Maelfu ya abiria walikusanyika kwenye kituo hicho wakijaribu kupanda treni zilizochelewa.

Kati ya waathirika hao, wanne walikuwa watoto, na wengine wakiwa ni wanawake. tukio hili limetokea wakati ambapo watu wakigombea kupata usafiri baada ya kuchelewa kwa treni nyingi.

Kupitia ukurasa wa X wa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ameeleza masikitiko yake ambapo amesema yupo pamoja na familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.

Ajali hii inajiri miezi michache tu baada ya tukio lingine la mkanyagano ambapo watu 30 waliuawa katika tamasha la kidini la Kumbh Mela, kaskazini mwa India.

Chanzo: NDTV

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button