TANGU kuanza kwa utalii wa matibabu mwaka 2021 takwimu za mwaka 2022 hadi Aprili ,2023 zinaonesha kuwa jumla ya wagonjwa 600 wamepatiwa matibabu ya kibingwa kutoka katika nchi mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Kmati ya Utalii wa Matibabu Taifa, Profesa Mohamed Janabi wakati wa Uzinduzi wa Sekretariet ya Utalii wa Matibabu katika Hospitali nne za Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI)Taasisi ya Saratani ya Ocean Road(ORCI) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa(MOI).
Prof Janabi amesema kupitia utalii wa matibabu pia madaktari wa Tanzania wamekuwa wakienda nchi mbalimbali kutoka huduma ambapo sasa madakatri kutoka JKCI wameenda Malawi kutoa huduma za upasuaji wa moyo.
“imefika mahali sisi tunaweza kusaidia wengine lakini pia tulipeleka madaktari Rwanda kwaajili ya upasuaji ambapo walifanya operation 25 mwaka 2021 imefika hatua sasa tunaweza kufundisha nchi jirani,”amesistiza Prof Janabi.
Amesema Kwa miaka 10 sasa uwekezaji wa serikali umepunguza kwa kiasi kikubwa upelekaji wa wagonjwa nje kwa asilimi 95 na tunaendelea kufanya hivyo.
“Sasa nia yetu ni kuwa kivutio na kuweza kuchangia lengo katika watalii milioni tano kufikia mwaka 2030 tuwe na watalii 500,000 kwaajili ya matibabu na kati yao watatu,wanne wanaweza kuugua na wawe na uhakikika tiba,”amesema.