MAMLAKA ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya imeepusha watu milioni tano katika matumizi ya dawa za kulevya.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema kuanzia Mwenzi Machi hadi Juni mwaka huu, DCEA ilikamata watuhumiwa 109 wakiwa na Dawa za Kulevya mbalimbali zikiwemo Heroin, Cocaine, Bangi kavu, Bangi mbichi, Bangi iliyosindikwa (Skanka) na kuteketeza ekari 1,093 za mashamba ya bangi
Amesema kiasi cha Heroin kilichokamatwa kati ya Machi 25, 2023 hadi Juni 19, 2023 iwapo kingeingia sokoni, kingeweza kutumiwa na kuathiri watu milioni 4.815