Watu wenye ulemavu watakiwa kupiga kura

MOROGORO: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imewashauri watu wenye ulemavu waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, mwaka huu kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachangua viongozi watakao wanawafaa kuwaletea maendeleo yao na taifa.
Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa huo, Christopher Mwakajinga ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya utoaji elimu ya kuwajengea uelewa juu ya masualaya rushwa yenye kauli mbiu: ‘Kataa Rushwa katika Uchaguzi“ kwa viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani Morogoro.
Mwakajinga amesema ushiriki wa makundi ya watu wenye mahitaji maalum katika uchaguzi si hisani bali ni haki yao ya msingi inayotokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo wanapaswa kushiriki uchaguzi mkuu kikamilifu bila kuwa na vikwazo vyovyote.
Amesema katiba yetu inatoa fursa kwa watanzania wote ambao wametimiza miaka 18 kuwa na haki ya kushiriki kwenye uongozi wa nchi na imetolewa bila kujali ulemavu wa mtu ,vipato vyao, ,hivyo wanapaswa kuitumia sawa na watanzania wengine wasio na ulemavu.
Mwakajinga amesema elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa juu ya hali za kisiasa za watu wenye mahitaji maalumu na ulemavu, kujenga ushirikiano kwa wadau ,Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ,Serikali na vyombo vyake vyote ikiwemo Takukuru ili kupambana na rushwa katika uchaguzi.
“ Ni lazima tuwekeane mazingira huru na sawa ili muweze kulitumia zoezi hili la msingi la haki ya kupinga kura,“amesema Mwakajinga .
Mwakajinga amewataka wawakilishi waliopatiwa elimu hiyo wajitokeze kushiriki kupinga kura na kuwahamsisha wenzao ili wawe chachu ya mabadiliko kwa sababu uchaguzi mmoja unapofanyika ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.
“Kutokana na elimu hii, ninawaomba mkawe mabalozi wa kuwaelimisha wengine , kwani kuelimika kwao juu ya masuala ya rushwa ni manufaa makubwa kwa taifa,” amesema Mwakajinga .
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu kwa nyakati tofauti ,waliwasishi wenzao wasishawishike na kurubuniwa kuchagua viongozi wa shinikizo la kupewa chochote.bali watumie haki yao kuchagua viongozi wanaowataka ili wawaletee maendeleo yao na Taifa na watakaodumia amani ya nchi yetu.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro wa Chama cha Wenye Ualbino (TAS) , Richard Lukwili pamoja na Salumu Ally mwenye usikivu hafifu wamesema elimu waliyoipata imewasidia kujua mambo ya rushwa katika uchaguzi hivyo watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ili waweze kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Kwa upande wake Kaimu Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro ,Amisa Kagambo aliipongeza Takukuru mkoa kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum kwa sababu ni kundi Muhimu katika Jamii.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com