Watu zaidi ya milioni 475 China wanatumia simu za 5G

IDADI ya watumiaji wa simu za 5G nchini China ilifikia milioni 475 mwishoni mwa Julai, mwaka huu kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari (MIIT).
Idadi hiyo ilisajili ongezeko la jumla la watumiaji milioni 120 ikilinganishwa na Desemba 2021, Ofisa wa MIIT aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.
Hadi kufikia mwisho wa Julai, nchi ilikuwa imejenga takribani vituo milioni 1.
97 vya msingi vya 5G, kwa miji yote ya ngazi ya wilaya, kaunti na asilimia 96 ya majiji yalikuwa na mtandao wa 5G, kulingana na MIIT.
Ujenzi wa miundombinu mipya ya mitandao ya 5G na mkongo utaendelea kupewa kipaumbele, MIIT ilisema. Juhudi pia zitafanywa ili kupanua wigo wa mitandao ya hali ya juu hadi maeneo ya vijijini, na kupanua kikamilifu matumizi ya njia mpya za biashara katika maeneo ya vijijini, wizara ilisema.