Watumia pombe ya kienyeji kunasa wadudu waharibifu

KITUO cha Utafiti wa Zao la Kahawa (TacRI) mikoa ya nyanda za juu, kilichopo Mbozi mkoani Songwe kimebuni teknlojia mpya ya kutumia pombe ya kienyeji kunasa wadudu waharibifu wa zao hilo.
Akizungumza na HabariLEO katika maonesho ya Nanenane jijini Mbeya, Meneja wa kituo hicho na mtafiti wa zao hilo, Dismas Panglas amesema walifanya tafiti na kubaini kuwa baadhi ya wadudu waharibifu wanavutiwa na harufu ya pombe, hivyo wao kubuni mitego ya kuwakamata kirahisi.
Meneja TaCRI Dismas Panglas ,akielezea tecnolojia ya mitego ya asili ya kutumia mimea ya asili aina ya utupa na mitego ya kutumia pombe za kienyeji kunasa wadudu waharbifu. (Picha zote na Baraka Messa)
“Tunachukua chupa za maji ndani yake tunaweka pombe za kienyeji ambazo huwavutia wadudu waharibifu na kuja kunaswa kwa kutumbukia kwenye ile chupa ya maji tuliyoikata na kuweka maji yaliyochanganyikana na pombe kidogo,” amesema Panglas.
Amesema ekari moja ya shamba la kahawa linachukua mitego sita mpaka kumi kutegemea na ukubwa wa miche ya kahawa pamoja na ukubwa wa tatizo katika shamba husika.
Amesema kwa wadudu waharibifu aina ya Bungua ambao hutoboa miche ya kahawa na kuikausha, wanasisitiza wakulima kupanda mimea ya asili aina ya utupa, ambayo hutwangwa na kupulizia kwenye miche ya kahawa na kuua wadudu hao.
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *