DAR-ES-SALAAM: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka watumishi serikalini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na misingi ya utoaji wa huduma ili kuleta matokeo chanya na sio kuwakwamisha watu wanaohitaji huduma.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo wakati akizindua Sera yaTaifa ya Biashara katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es alaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi.
“ Tunaweza kuwa wazuri sana wa kuandika kutoa matamko na kutoa ahadi lakini hali halisi haibadiliki, Hakuna faida ya kuwa na afisa anayejipanga kumkwamisha mfanyabiashara ili tu aitwe bosi, Tunatakiwa kuwa na nyaraka inayotuunganisha wote vinginevyo sera hii itabaki kuwa kitabu cha hadithi kwenye kabati,” Amesema Dkt.Biteko
Amewahimiza watumishi serikalini kuwahakikishia watu wote wanapata huduma hizo pasipo kuwekewa vikwazo suala ambalo litawajengea heshima mbele za watu wanaotafuta huduma hizo, “Uwepo wa sera ya taifa ya biashara utasababisha mabadiliko makubwa katika nyaraka na sheria mbalimbali za nchi na hivyo sekta zote za serikali zinatakiwa kuisoma sera hii na kuisimamia.“ amesema Dkt. Biteko
Katika hate nyingine, Dkt. Biteko amewataka watanzania kutumia fursa ya Sera hii kuwa nyezo ya kuimarisha nguvu za kiushindani kitaifa, kikanda na kimataifa huku akiainisha hifadhi ya mazingira na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Aidha amewataka watanzani kutembea kifua mbele wakiamini kuwa wanao uwezo wa kushindana na kushindanisha bidhaa kwa kuboresha bidhaa hizo ili kuvutia masoko ya ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia kuwa sera hii ni ya biashara na siyo sera ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Dkt. Biteko pia amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan haipendi kuona ama kusikia kero dhidi ya wafanyabiashara hivyo, wadau wote wana ni umuhimu kutumia fursa hiyo kuboresha huduma kupitia sera hii mpya.
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe, Dkt. Selemani Jafo amesema mabadiliko ya kibiashara duniani yanasababisha mabadiliko ya biashara na mitaji kuwawezesha watanzania kushiriki katika ujenzi wa Uchumi.
SOMA: Simbachawene aonya maadili yasiyofaa kwa Watumishi
Kwa upande wake, Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Tone Tinnes amesema ni wazi kuwa Tanzania imekuwa kivutio cha biashara na imeongeza mauzo ya bidhaa zake poamoja na uwekezaji wa mitaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchini.