Waungana upatikanaji umeme visiwa vya Ziwa Victoria

ARUSHA: KAMPUNI ya PowerHut Renewables Limited yenye makao yake mjini Arusha imeingia katika mkataba wa mwaka mmoja wa ushirikano wa kimkakati baina yake na shirika la Assist International na Kampuni ya Caterpillar Inc zote za Marekani pamoja na Mantrac ya Tanzania kuunga mkono upatikanaji wa umeme wa uhakika, gharama nafuu, endelevu, jumuishi na nishati safi ya kupikia kwa wote.
Ushirikiano huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme katika visiwa vinne vya Juma, Kasalazi, Ziragula na Bezi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa PowerHut Renewables Limited, Dk Prosper Magali, ushirikiano huo utaboresha miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa umeme katika visiwa hivyo ili kumudu mahitaji ya nishati hiyo yanayoendelea kuongezeka visiwani humo hasa katika uzalishaji mali kwa kutumia umeme.
“Matamanio ya watu ya kuboreshwa kwa huduma za umeme sasa yanashughulikiwa,” anasema Dk Magali.
Katika taarifa ya pamoja, Makamu wa Rais wa Program na Mikakati wa Assist International, Cheri Reynolds anasema: “Umeme wa uhakika hujenga uwezekano mpya katika familia na jamii; huwezesha watoto kusoma hata giza linapoingia, vituo vya huduma za afya vinaweza kuhudumia wagonjwa kwa uhakika na biashara ndogo zinaweza kupanuka na kukua.”
Anaongeza: “Assist International imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania kwa miaka mingi na kushuhudia nguvu ya ubia katika kuleta mabadiliko endelevu. Tumevutiwa kujiunga katika ushirikiano huu kuleta nishati inayojitegemea kusaidia elimu, huduma za afya na ukuaji wa Uchumi.”

Yote haya yanafanyika kupitia Mpango wa Huduma za Umeme wa kampuni ya Caterpillar Inc (Caterpillar Electrification Initiative) ambao ni mpango wa uhisani unaolenga kupeleka huduma za umeme katika maeneo mbalimbali ya Afrika kwa kutumia teknolojia madhubuti za Caterpillar.
Mpango huu unasimamiwa na Assist International, shirika lisilo la kiserikali la nchini Marekani, linalosambaza shughuli za kimkakati na endelevu duniani kote zikiwemo huduma za nishati.
Makamu wa Rais wa Caterpillar Inc katika Kitengo cha Umeme, Mellissa Busen anasema: “Kupata umeme wa uhakika nchini Tanzania ni zaidi ya miundombinu, ni hasa kuwezesha jamii, kuimarisha usalama na kufungua fursa.”
Anaongeza: “Ushirikiano huu unaakisi kujitoa kwa Caterpillar na Mantrac kwa ajili ya Watanzania kuhakikisha tunachangia kujenga ulimwengu endelevu zaidi.”
Naye Meneja Usimamizi wa Biashara kwa Afrika Mashariki wa Mantrac Tanzania, Amr Zaki anasema: “Tunaona fahari kuunganisha nguvu na kampuni za PowerHut, Caterpillar na Assist International kuleta suluhisho endelevu la nishati ili kusaidia mabadiliko ya maisha na kuimarisha uhimilivu wa ndani.”
Kwa mujibu wa Dk Magali, miongoni mwa walengwa na wanufaika wakuu wa mradi huo ni wajasiriamali wakiwamo wa ufundi wa fani mbalimbali zikiwamo za useremala na uchomeleaji vyuma (welding).
Anasema mkakati huo unalenga kuwezesha wakazi wa visiwa hivyo kupata kirahisi na kutumia nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono juhudi za serikali kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia kulinda afya za watu na kukabili uharibifu wa mazingira.
“Moja ya maboresho hayo ni kuwezesha miundombinu hiyo kuchaji betri zinazotumiwa na wavuvi kuvua samaki na kuwezesha uhifadhi wa mazao ya samaki kwa kutumia miundombinu inayotumia umeme kama majokofu pamoja na kugandisha barafu kwa ajili ya kazi hiyo,” anasema Dk Magali.
Anaongeza: “Miongoni mwa mengi tutakayoyafanya ni kuwezesha upikaji kwa kutumia umeme ili kuepusha uharibifu wa mazingira na kurahisisha mchakato wa upikaji chakula nyumbani…”
“Ikumbukwe visiwani kuna changamoto kubwa ya kupata kuni na mkaa maana visiwa vingi havina kuni wala mkaa badala yake, wanategemea kununua kutoka nchi kavu.”
Katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Magali anasema: “Huu ni ukombozi dhidi ya madhara kwa wanawake na watu wengine yanayotokana na moshi utokanao na matumizi ya muda mrefu ya kuni sambamba na watu hao kutumia muda mwingi na gharama kubwa za fedha kutafuta kuni na mkaa badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali.”
Anaongeza: “Mpango utaboresha huduma za afya katika zahanati na maduka ya dawa, maabara ndogondogo kwa kutoa mwanga wakati wa kutoa huduma za afya zikiwamo za wajawazito kujifungua pamoja na kuhifadhi dawa na chanjo.”
Katika utekelezaji wa ushirikiano huo wa mwaka mmoja tangu Desemba 4, 2025, kampuni ya PowerHut Renewables Limited ndiyo inayomiliki na kushughulikia miundombinu na shughuli za kila siku za uzalishaji umeme na uendeshaji katika visiwa hivyo.
“Wadau wengine (kampuni hizo) kwa pamoja watatoa fedha na teknolojia katika kufanya uboreshaji unaokusudiwa. Tunatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini, wizara husika na taasisi zake na wadau wengine kuhakikisha mpango huu unatekelezwa kwa mafanikio na kunufaisha wananchi katika visiwa hivyo.”
Kampuni ya PowerHut Renewables Limited ina miradi minane ya kuzalisha na kusambaza umeme katika visiwa kwa kutumia umemejua (solar energy) na kuusambaza kwa kutumia gridi ndogo tangu mwaka 2018.
Miradi hiyo inatoa huduma ya umeme kwa wakazi zaidi ya 2000 katika visiwa vya Juma, Kasalazi, Ziragula, Bezi, Yozu, Chembaya, Sozia na Lyegoba vilivyoko katika Ziwa Victoria.
“Hata hivyo, tumebaini kuwa, mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na hivyo, kulazimika kutafuta na hatimaye kupata wadau wa kufanya uboreshaji unaokusudiwa ili kukidhi mahitaji ya watu,” anasema Magali katika taarifa hiyo.




Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
.
More Details For Us →→ http://www.big.income9.com
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com