Wawili wapoteza maisha ajali Kenya

WATU wawili wanahofiwa kufa baada ya gari la shule ya wavulana Kapsabet kupinduka katika Jimbo la Baringo nchini Kenya leo.

Taarifa ya mtandao wa NTV Kenya, iliyotolewa muda huu imeeleza kuwa waliokufa ni mwalimu na mwanafunzi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Nation, polisi imetaja chanzo cha ajali ni dereva kupoteza mwelekeo alipojaribu kukata kona na gari hilo kuangukia kwenye bonde.

Kamanda wa polisi eneo hilo, Stephen Kutwa amesema basi hilo lilibeba wanafunzi 61 na mwalimu mmoja. Hata hivyo majeruhi wamewahishwa hospitali.

Habari Zifananazo

Back to top button