Wazazi watakiwa kupeleka watoto shule

GEITA:Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameeleza kuwa, Serikali itawachukulia hatua wazazi wote  wasiopeleka watoto wao shule kupata elimu.

SOMA: Majaliwa: Wazazi fuatilieni watoto shuleni

Amewataka wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha wanawapeleka Watoto wao shule na wale wanaoleta ukinzani dhidi ya maelekezo hayo waripotiwe katika mamlaka za ngazi husika ili kutafuta suluhu ya tatizo hilo.

Advertisement

Hayo yamebainishwa wakati wa Mkutano wa hadhara akizungumza na wananchi kijiji cha Ilyamchele Kata ya Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

SOMA: https://www.moe.go.tz/